NEWS

29 Desemba 2016

Idadi ya malori yaliyositisha safari mwaka 2016 sababu ya kupungua kwa mizigo

Chama Cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) kimeeleza kuwa kwa mwaka 2016, jumla ya malori 15,000 yamesitisha kutoa huduma nchini Tanzania sababu kubwa ikiwa ni kupungua kwa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa takwimu walizozitoa zilizonyesha kuwa jumla ya malori 20,000 yalikuwa yakitoa huduma za usafirishaji wa mizigo katika nchi mbalimbali lakini mengi yamesitisha safari zao.

Chama hicho kilisema kuwa kati ya mwaka 2010 na 2015 walifanyabiashara vizuri kabisa lakini baada ya hapo hali imekuwa mbaya sababu mizigo imepungua kufuatia waingizaji wa bidhaa nchini Zambia kupitia bandari ya Dar es Salaam, wameihama bandari hiyo. Sababu ya wafanyabiashara wa Zambia kupunguza kutumia bandari ya Dar es Salaam imeelezwa kuwa ni gharama kubwa.

Biashara ya usafirishaji hailipi tena kama zamani na pia gharama zimekuwa kubwa sana hivyo Zambia wakaamua kutumia bandari ya Durban, Beira na Walvis.

Kufuatia magari hayo kusitisha safari zake, mbali na madereva na utingo lakini pia Mama N’tilie, wamiliki wa nyumba za kulala wageni, wafanyakazi wa bandari nao wamejikuta wakipoteza kazi zao.

The post Idadi ya malori yaliyositisha safari mwaka 2016 sababu ya kupungua kwa mizigo appeared first on SWAHILI TIMES.