NEWS

30 Desemba 2016

Picha 5: Waziri Mwigulu Nchemba atembelea ofisi za WCB

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba ametembelea ofisi wa WCB zilizopo Tandale jijini Dar es Salaam ambapo alipata nafasi ya kufanya mazungumzo na uongozi na wasanii waliopo chini ya WCB.

nchemba

Mbali na mambo mengi wambayo Waziri Nchemba aliahidi alipofanya nao mazungumzo ni kuhusu Jeshi la Polisi kuongeza nguvu kwenye upambanaji dhidi ya kazi za wasanii.

1

Alisema anafahamu kuwa wasanii wamekuwa wakiibiwa kazi zao na hivyo kukosa kiasi kikubwa cha fedha na hivyo Jeshi la Polisi nchini kote litahakikisha kuwa linapambana kuzuia hali hiyo.

Kwa upande wa WCB wamemshukuru Waziri Nchemba kwa kutembelea ofisi hizo na kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwao kwani utasaidia kuwaendeleza na kukuza sanaa ya Tanzania kwa ujumla.

2 3

 

 

The post Picha 5: Waziri Mwigulu Nchemba atembelea ofisi za WCB appeared first on SWAHILI TIMES.