Jakaya kikwete alikuwa kiongozi wa nchi yetu aliyejitahidi sana kutoa uongozi bora unaozingatia sheria za nchi na kuleta maendeleo katika nchi yetu .
Alijitahidi sana kuboresha hali za maisha ya watu kwa kuongeza kipato na kutengeneza mazingira mazuri ya biashara .
Aliongeza stahiki kwa watumishi wa umma na kuwafanya wakopesheke kwa ajili ya maendeleo .
Aliongeza upatikanaji wa umeme na maji kote nchini hadi vijijini .
Alihakikisha kila mtu anapata fursa ya kusoma kadri ya uwezo wake .
Tukashuhudia maendeleo makubwa katika Huduma za afya na miundombinu kuanzia barabara hadi viwanja vya ndege .
Itoshe tuu kusema alifanya mengi mazuri ya kupigiwa mfano kwa nchi yetu .
Ni kweli yalikuwepo mapungufu mengi katika utawala wake lakini Mapungufu yalikuzwa mazuri yakadhoofishwa .
Juhudi kubwa zilifanywa kuonesha kuwa ni kiongozi asiyefaa hata kidogo na aina yake ya utawala nayo haifai .
Hila na chuki zikapandikizwa juu yake .
Nyumba za ibada zikatumika kumdhoofisha na kudhoofisha utawala wake .
Tukashuhudia manyaraka yakitolewa kila mara kuikosoa na kuikaripia serikali yake ?
Leo najiuliza Nyaraka zile ziko wapi kama kweli walikuwa wanafanya vile kwa dhamira njema na uzalendo kwa nchi ?
Hakuna Kingine isipokuwa walikuwa wanafanya vile kwa hila na chuki .
Ndio maana ukosoaji wao una msimu .
Nakumbuka wakati anaaga ccm alisema "Historia itatoa hukumu iliyo ya haki ".
Leo waliokuwa wanambeza na kumkashifu sasa wanaongoza kumsifu na kumpongeza .
Ili tujenge nchi yetu ni lazima kuwa wazalendo na kuepuka hila na chuki .
Tunawajibu wa kuwakosoa viongozi wetu lakini tusifanye hivyo kwa hila na chuki tufanye hivyo kwa dhamira njema na mapenzi kwa nchi yetu .
" Tukipanda mbegu za hila na chuki tutavuna matunda ya hila na chuki ".