NEWS

6 Juni 2017

AT: “Ugomvi wa Alikiba na Diamond ulianzia Oman 2010, mimi Shahidi”


Mwimbaji staa wa miondoko ya Mduara AT amefunguka kwenye XXL ya Clouds FM na kudai kuwa aliwahi kushuhudia ugonvi wa Alikiba na Diamond ambao kwa mujibu wake ulianzia Uarabuni naye alikuwa shahidi.

AT amesema watu wengi wanakurupuka kuhusu ugomvi wa Alikiba na Diamond kwa kuwa alikuwepo Oman mwaka 2010 ambapo Alikiba na Diamond walikuwa wanacheza Game chumbani kwake kwenye Hotel waliyofikia.

“Tulikuwa Oman kwenye Hotel moja. Tulikuwa na Show, sasa walikuwa wanacheza Game Alikiba na Diamond huku Alikiba akiwa amechagua Real Madrid na Diamond amechagua Barcelona. Alikiba akilikuwa amefungwa mbili, Diamond tatu.

“Kwa hiyo Alikiba alikuwa nataka kupiga free-kick kwenye game Diamond akamsukuma Alikiba na Alikiba akastopisha game akamwambia kuwa mwanangu nilikuwa nakutafuta muda mrefu sana ikabidi mimi ninyanyuke sasa niwaamue.” – AT