NEWS

6 Juni 2017

Rihanna Awajia Juu Waliomuita Kibonge


Msanii wa muziki Rihanna amewajibu watu wanao mkejeli kwa kumuita kibonge nyanya.

Wiki iliyopita watu walisambaza picha mitandaoni zikimuonyesha mrembo huyo jinsi alivyonenepa na huku wengine wakihisi ni mjamzito na wengine wakimuandikia maneno ya kashfa..

Hata hivyo Rihanna ameamua kukata mzizi wa fitina na kuamua kuwajibu kupitia mtandao wa Instagram, kwa kupost picha ya Gucci Mane enzi zake alivyokuwa mnene na ile ya sasa hivi inayomuonyesha amepungua zaidi na kuweka picha ya mdoli akiwa analia.