NEWS

7 Juni 2017

Tanzania yashiriki Mkutano wa kujadili matumizi ya Bahari na rasilimali zake

Ujumbe wa Tanzania unaoongozwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Charles Tizeba ukiwa kwenye mkutano wa utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu Na. 14 (Sustainable Development Goals-SDGs14) maarufu kama Oceans Conference unaojadili matumizi endelevu ya bahari na rasilimali zilizomo baharini, unaoendelea Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekan. 
Waziri wa Kilimo, Nifugo na Uvuvi, Mhe. Charles Tizeba akiwasilisha hotuba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania kwenye Mkutano wa Kimataifa wa kuweka mikakati ya utekelezaji wa SDG14 unaoendelea Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekan. Mkutano huo ni maalum kwa ajili ya kujadili kuhusu matumizi endelevu ya bahari na rasilimali zilizomo baharini kama sehemu ya utekelezaji wa lengo la 14 la malengo ya maendeleo endelevu.