Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza kabla ya kuongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa marehemu, Muhingo Rweyemamu mcahan wa leo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Marehemu Muhingo Rweyemamu amezikwa leo kwenye makaburi ya Kinondoni.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitoa neno wakati wa kumuaga Mwandishi wa habari mkongwe nchini, Muhingo Rweyemamu yaliyofanyika leo Uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mtoto wa marehemu akisoma risala.
Mwili wa marehemu mwandishi wa habari mkongwe nchini, Muhingo Rweyemamu ukiwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.