NEWS

20 Februari 2018

2nd Half: Gendarmerie 0 – 1 Simba

Klabu ya Simba wakiwa ugenini nchini Djibouti wanaongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Gendarmerie, bao la Simba likiwekwa langoni na mshambuliaji wa Kimataifa Raia wa Uganda, Emmanuel Okwi dakika ya 53 ya mchezo huo.
Mechi hiyo imekuwa na ushindani mkubwa na Simba wamepoteza nafasi za tatu za kufunga za wazi huku wenyeji Gendamerie wakipoteza moja katika kipindi cha kwanza pekee.
Simba wameonekana kushambulia lakini Gendamerie wako makini nao wamekuwa wakijibu mashambulizi tofauti na mechi ya kwanza ambayo walifungwa kwa mabao 4-0 mjini Dar es Salaam.

The post 2nd Half: Gendarmerie 0 – 1 Simba appeared first on Global Publishers.