NEWS

19 Februari 2018

Ali Kiba Aamua Kufuata Nyayo za Ben Pol...Atupia Marangi Rangi Kichwani

Imekuwa ni kawaida kwa mastaa mbalimbali Duniani kupenda kubadili mionenakano yao, inawezekana ukawa ni muonekano wa style za mavazi au wakati mwingine inaweza ikawa style za nywele ili tu kuwa tofauti.

Kuna mitindo ya nywele kwa baadhi ya mastaa inayo-trend  ambapo kwa sasa kila mtu anakuja na mtindo wake mwenyewe ili kuleta upekee wa muonekano wake kama ilivyo kwa Ben Pol alikuja na mtindo wa rangi ya nywele za kijani kibichi na imempa dili kibao kutokana na mtindo huo wa rangi.

Staa wa Bongofleva Ali Kiba leo nae ameonekana akiwa miongoni mwa mastaa wa Bongo waliokuja na style mpya wa nywele ambapo ameamua kuweka rangi ya kwenye nywele zake na kuubadili muonekano wake kichwani tofauti na tulivyomzoea.