NEWS

16 Februari 2018

Kauli ya Chadema Kuhusu Taarifa Inayosambaa Kuwa Wamejitoa Uchaguzi wa Kesho

CHADEMA cha Demaokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekanusha taarifa inayosambaa mitandaoni kuwa wamejitoa kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge kwa majimbo ya Kinondoni na Siha unaotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi, Feb 17, 2018.

 

Akizungumza na Global Publishers, jioni Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene amesema taarifa hizo si za kweli na kwamba zimeandaliwa ili kuwapotosha wapiga kura. 

Naye Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema;

“Kuna barua inasambazwa kwenye Mitandao kuwa CHADEMA imejitoa kwenye uchaguzi wa Majimbo ya Kinondoni na Siha, hizi ni propaganda dhaifu za waliokwisha kushindwa, wanafanya hivi kuwakatisha tamaa wapiga kura ili wasijitokeze kesho kupiga kura, wapuuzeni hao.

 

“Hawajui hata utaratibu kuwa ni mgombea tu ndio mwenye haki ya kuandika barua ya kujitoa na sio M/Kiti wa Chama. Mbowe anafunga kampeni Kinondoni muda huu na mzee Lowassa anafunga Kampeni Siha Muda huu.”

 

The post Kauli ya Chadema Kuhusu Taarifa Inayosambaa Kuwa Wamejitoa Uchaguzi wa Kesho appeared first on Global Publishers.