MTUMISHI wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Hassan Abuutwalib maarufu Kiringo anashikiliwa na Jeshi la Polisi Zanzibar kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 13.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Hassan Nassir Ali amesema wamemkamata jana Februari 18, 2018 katika maeneo ya Uwanja wa Ndege Zanzibar alipokuwa akijaribu kuondokea Mwanza.
Kamanda Nassir amesema Kiringo anatuhumiwa kumlawiti mtoto wa miaka 13 baada ya baba wa mtoto huyo jina limehifadhiwa mwenye miaka 54 kuripoti polisi kuwa mtoto wake alichukuliwa na Kiringo na kumpeleka katika nyumba iliyokuwa haijamalizwa kujengwa huko Fuoni Uwandani ambapo alimlawiti baada ya kumpa dawa za kupoteza fahamu na kumsababishia maumivu makali ambapo ripoti ya uchunguzi wa madaktari ilithibitisha kuathirika sehemu za siri za nyuma za mtoto huyo.
Aidha, Kamanda Nasiri amesema ameunda timu ya uchunguzi iliyojumuisha wakuu wa upelelezi wa wilaya tatu Wilaya ya Mjini, Wilaya ya Magharibi A na B kufanya uchunguzi juu ya suala hilo zito ambalo ameshindwa kulifumbia macho.
Kiringo aliwahi kushutumiwa kwa matukio tofauti ya kulawiti kabla ya tukio hili, wananchi wamekuwa wakipiga kelele kwa kuwaharibia vijana wao.
Akwilina alifariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi kichwani akiwa kwenye daladala wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chadema.
The post Kigogo wa TRA Mbaroni, Adaiwa Kumlawiti Mtoto wa Miaka 13 appeared first on Global Publishers.