NEWS

26 Februari 2018

Mastaa Walivyoguswa na Kifungo cha Sugu

KUFUATIA Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga kuhukumiwa jela miezi mitano kwa kosa la kutumia lugha ya fedhea dhidi ya Rais Magufuli, baadhi ya mastaa nchini wakiwemo wasanii wa bongo fleva, wamefunguka na kuonyesha kuguswa na tukio hilo huku wengine wakimtia moyo kuwa gerezani siyo kaburini hivyo atamaliza muda wake na kurudi uraiani kuwapigania wananchi wa Mbeya.

 

Niki wa Pili: Nguvu ya Mungu ikapate kuwa nawe pamoja na familia yako, gerezani sio kaburini ‘stay strong’ Jongwe.”

Nay wa Mitego: Stay Strong Brother Sugu

Rama Dee: Nasikitika sana kwa hii habari kama msanii pia kama rafiki wa Sugu, hii si picha nzuri.

Izzo Izness: Stay strong Big Brother JONGWE

Roma Mkatoliki: Hata hili lipatita’ stay strong Joseph Zaburi 35: 1-28.

 

The post Mastaa Walivyoguswa na Kifungo cha Sugu appeared first on Global Publishers.