NEWS

26 Februari 2018

MAHAKAMA YAITUPA KESI YA MCHUNGAJI MWINGIRA

Mchungaji Josephat Mwingira.

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeitupilia  mbali kesi ya madai iliyofunguliwa na Dkt. William Morris, raia wa Marekani dhidi ya mkewe Phills Nyimbi na Mchungaji Josephat Mwingira na kutaka alipe gharama alizotumia mdaiwa.

 

Dkt. William Morris aliwasilisha maombi mahakamani hapo akiomba mkewe, Mwingira na mtoto wake (9) wafanyiwe kipimo cha kujua vinasaba  vya mtoto (DNA).

 

Dkt. Morris ambaye ni mume wa (mdaiwa wa pili, Phills Nyimbi) aliiomba mahakama itoe amri ya mkewe, Mwingira na mtoto wakafanyiwe kipimo hicho cha DNA ili aweze kujua wazazi  halisi wa mtoto aliyezaa na mkewe.

 

Alidai mchungaji Mwingira alizini na mkewe na hatimaye kuzaa naye mtoto wa huyo wa kiume.

 

Akisoma hukumu hiyo leo Februari 26,  Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, amesema Dkt.  Morris katika kesi hiyo ameshindwa kuonyesha mahusiano ya kimapenzi  kati ya Phills na Mchungaji Mwingira.

 

Pia ameshindwa kuthibitisha kuwa mtoto aliyezaliwa na mke wa  Morris ni matokeo ya  mahusiano ya kimapenzi  kati ya Phills na Mchungaji Mwingira.

 

Hivyo mahakama imeitupilia mbali kesi hiyo na kusema mdai ameshindwa kuthibitisha madai yake  katika kiwango kinachotakiwa katika mashauri ya madai na alipe gharama.

 

Desemba 28, 2011,  Morris na Phills  walifunga  ndoa  ya kanisani  na wakati wa mahusiano yao, Phills  na Mchungaji Mwingira wanadaiwa  kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na kupata  mtoto wa kiume.

 

Na Denis Mtima/GPL.

 

 

 

The post MAHAKAMA YAITUPA KESI YA MCHUNGAJI MWINGIRA appeared first on Global Publishers.