KIKOSI cha Yanga, leo Jumatano kinashuka uwanjani kupambana na St Louis ya Shelisheli katika mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Afrika, huku kikiwakosa nyota wake wanne wa kigeni kutokana na majeraha
Kwenye mchezo huo muhimu, Yanga itamkosa, Obrey Chirwa, Amissi Tambwe, Donald Ngoma pamoja na Thaban Kamusoko.
“Yanga hawana haja ya kuwa na wasiwasi na wachezaji watakaocheza dhidi ya St Louis, kwani ni wacheza wazuri na wenye uwezo kufanya vizuri endapo wataamua kupambana.
“Nasema hivyo kwa sababu ninawajua vizuri, baadhi yao wana uwezo mkubwa kushinda hata sisi tuliobaki huku ila tu tunachowashinda sisi ni uzoefu lakini wakiamua kupambana ushindi utapatikana na ninaamini itakuwa hivyo,” alisema Tambwe ambaye amewahi kutamba na Simba.
Stori na Sweetbert Lukonge | Global Publishers
The post Tambwe: Yanga Inavuka Leo, Wala Msiogope appeared first on Global Publishers.