NEWS

21 Februari 2018

TANZANIA YAONGEZEWA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA

 

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa), limeamua kuongeza tiketi za kwenda kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Urusi mwezi Juni, mwaka huu. Mwisho wa mauzo ya tiketi hizo ni mwezi ujao.

Akizungumza na Championi Juma­tano, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, alisema kuwa Fifa wameamua kuongeza idadi ya tiketi za Kombe la Dunia pamoja na kuongeza muda wa kununua tiketi hizo.

 

“Kuna mambo matatu ambapo la kwanza ni kuhusu ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho la FA ambapo ke­sho (leo) utachezwa mchezo mmoja kati ya Njombe Mji na Mbao kwenye Uwanja wa Sabasaba lakini mechi zake zitaen­delea Jumamosi ambapo Singida United watawakaribisha Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Namfua na KMC watacheza na Azam kwenye Uwanja wa Azam Complex lakini Jumapili kutakuwa na Buseresere watacheza na Mtibwa, pia kutakuwa na mechi ya Majimaji dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Majimaji.

 

“Jambo la pili ni kuhusu ratiba ya Ligi Kuu Bara mchezo wa Ndanda dhidi ya Yanga ambao haukupangwa tarehe, utachezwa Februari 28 huku Simba dhidi ya Mbao wao watacheza Februari 26, lakini mwisho ni Fifa wameamua ku­tuongezea tiketi za kwenda kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia ambapo awali zilikuwa tiketi 290, zilizoongezwa hazina idadi kamili , pia wameongeza na muda wa mauzo ya tiketi hizo hadi Machi 12, kama kuna watu wanahitaji wawasiliane na TFF,” alisema Ndimbo.

 

Ibrahim Mressy na Lunyamadzo Mlyuka

The post TANZANIA YAONGEZEWA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA appeared first on Global Publishers.