Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine sita wa chama hicho wameitwa na Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu tuhuma zinazowakabili za kufanya maandamano kinyume cha sheria.