NEWS

25 Februari 2018

Wasomaji Wa Spoti Xtra Wazawadiwa

Wasomaji wa gazeti la Spoti Xtra walionunua gazeti hilo kwenye msafara wa promotion uliokuwa ukipita viunga mbalimbali vya jiji la Dar, jana Jumapili walizawadia zawadi mbalimbali ikiwemo sabuni, dawa za meno na nyinginezo.

Katika promotion hiyo wasomaji wa magazeti ya burudani na michezo waliendelea kulisimfia gazeti hilo kutokana na ubora wa habari zake na makala zilizochambuliwa na waandishi wazoefu.

Wasomaji hao walipatiwa nafasi ya kutoa maoni yao ambapo walitoa maoni mbalimbali ambayo yanatarajiwa kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.

Msafara huo ulikatiza katika viunga mbalimbali vya jiji la Dar ambapo ulianzia Sinza Mori, na kuelekea Mwenge, Manzese Kwa Mfuga Mbwa, Soko la ndizi mabibo, Kigogo Luhanga, Kigogo Mwembe Jando, Tabata Dampo na maeneo mengine ambapo maeneo yote hayo wasomaji walionunua gazeti hilo walipewa zawadi.

Stori na  Richard Bukos| Global Publishers

The post Wasomaji Wa Spoti Xtra Wazawadiwa appeared first on Global Publishers.