NEWS

31 Mei 2018

ALICHOKISEMA KIKWETE KWA KINANA, JPM

RAIS mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete,  amempongeza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, kwa kazi nzuri aliyoifanya ndani ya chama wakati wa uongozi wake huku akimtakia kila la kheri katika maisha yake baada ya kustaafu wadhifa wake huo.

Kikwete amempongeza pia Dkt. Bashiru Kakurwa kwa kuteuliwa na Kamati Kuu ya CCM juzi kuwa Katibu Mkuu  wa chama hicho kuchukua nafasi ya Kinana.

 

Aidha, amempongeza Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli kwa kukiendesha vyema chama hicho huku akiwataka wanachama wake waendeleze umoja wao.

Kwa heri Kinana. Hongera kwa kazi nzuri. Daima tutakukumbuka. Hongera Bashiru. Nakutakia kila la heri. Hongera , hongera Mwenyekiti Umoja ni Ushindi, Kidumu Chama Cha Mapinduzi !

The post ALICHOKISEMA KIKWETE KWA KINANA, JPM appeared first on Global Publishers.