MBALI na kumtambulisha mchezaji wao mpya raia wa Brazil, Felipe Olveira Dos Santos, Klabu ya Singida United, hiyo imewatambulisha wachezaji wengine wawili ambapo mmoja ni Amara Diaby, raia wa Ivory Coast aliyetokea Klabu ya Asec Mimosa nchini humo ambako anatokea nyota wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba.
Utambulisho huo umefanywa na Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga wakati akizungumza na wanahabari jijini Arusha leo. Singida United pia imemtwaa Tiba John kutoka Ndanda FC aliyesaini miaka mitatu.
George amejiunga na matajiri hao wa mjini Singida akitokea Ndanda FC kutoka Mtwara iliyojikwamua kuepuka kushuka daraja msimu uliomalizika.
Wote watatu wametambulishwa jijini jijini Arusha, wakiwa tayari kwa ajili ya Fainaly ya Kombe la Shirikisho la Azam (FA) watakapocheza na mtibwa Sugar, Jumamosi hii, Juni 2, 2018 na baadaye kuelekea Kenya michuano ya SportPesa Super Cup.
The post ‘NDUGU WA DROGBA’ ATAMBULISHWA SINGIDA UNITED appeared first on Global Publishers.