NEWS

30 Mei 2018

Vodacom Yasherekea Miaka 10 Ya Mafanikio Ya M-Pesa Nchini

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao.

 

KAMPUNI  ya Simu ya Vodacom Tanzania imefanya hafla fupi ya kusheherekea na kuadhimisha mafanikio ya miaka 10 ya huduma yao ya M-PESA iliyosambaa nchi zima. Maadhimisho hayo yamefanyika makao makuu ya Vodacom yaliyoko Morocco jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom,  Ian Ferrao amesema mwaka 2008 walizindua huduma ya M-Pesa.

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao (katikati) akimkabidhi mmoja ya wadau wa M-Pesa tokea ilipozinduliwa na Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia.

 

Amewapongeza watanzania kwa kuipokea huduma hiyo ya M-pesa na imechangia kukuwa kwa uchumi wa watumiaji kwa kutumia huduma hiyo kufanya malipo ya vitu mbalimbali, kupokea pesa kutoka kwa mtu yeyote aliyeko popote ndani ya Tanzania na nche ya nchi.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia akiongea na wanahabari (hawapo pichani).

Pia mkurugenzi huyo amesema kuwa kupitia Mpesa kwa sasa unaweza kulipia huduma mbalimbali kama kulipia huduma za vigamuzi, huduma ya maji, huduma ya luku, marejesho ya mikopo,  huduma za elimu, bima, kununua vifurushi na vocha, Kutoa na kuweka pesa benki pamoja na kutuma pesa mitandao mingine.

The post Vodacom Yasherekea Miaka 10 Ya Mafanikio Ya M-Pesa Nchini appeared first on Global Publishers.