NEWS

20 Agosti 2018

Baba Jokate Awafunda Wema Sepetu na Irene Uwoya


Baba mzazi wa Msanii na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate, Mzee Urban Costa Ndunguru amefichua siri nzito inayowafanya mpaka Wema Sepetu na Irene Uwoya Wasafikie malengo yao kisiasa.

Kwenye mahojiano na gazeti la ‘Amani’ Nduguru aliliambia Amani katika mahojiano maalum kwa njia ya simu hivi karibuni kuwa:

Mwanangu, Wema, Uwoya wote wana ndoto za kuwa wanasiasa na viongozi wa umma lakini hawa wawili kuna mambo yanawakosesha fursa.

Mimi Uwoya simfahamu sana, namsikia tu habari zake kwenye magazeti, lakini Wema namfahamu kwa sababu baba yake (marehemu Isack Sepetu) nimefanya naye kazi serikalini.

Matatizo yanayowakosesha nafasi za kufikia ndoto zao hawa watoto yako mengi lakini kubwa kabisa ni kuiacha misingi bora waliyolelewa na wazazi wao. Siri kubwa ya kufanikiwa hasa katika kutumikia watu ni kujiheshimu na kufanya mambo kwa siri, siyo kwenda kiholelaholela, unajivunjia heshima mwenyewe”. Lakini pia Baba Jokate amewataka warembo hao wawili kuiga mfano wa Jokate:

Nimeona wanampongeza mwanangu kwa kuteuliwa kwake (kuwa DC), na mimi nasema wasiishie kumpongeza tu lakini waige tabia zake.

Jokate ni mwanangu, sisemi ni mkamilifu lakini ni msiri sana, vigumu kumuona kwenye jamii akifanya vitu vya ovyo, tabia hii naomba Wema na Uwoyawaiige itawasaidia kufikia ndoto zao za kuwa viongozi“.