NEWS

23 Agosti 2018

Breaking News: Bobi Wine Aachiwa Huru, Besigye Akamatwa

Taarifa za hivi punde kutoka Uganda ni kwamba mahakama ya jeshi imemuondolea mashtaka mbunge wa Kyadondo Robert Kyagulanyi.

Inaarifiwa kwamba mahakama hiyo ya jeshi inataka badala yake kumkabidhi mbunge huyo kwa mahakama ya kiraia ajibu mashtaka ya uhaini pamojana wabunge wengine waliokamatwa.

Mbunge huyo ambaye aliwahi kuwa mwanamuziki nchini kwa jina maarufu Bobi Wine leo alitarajiwa kurudishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda.

Mawakili wake awali walijuzwa kuwa kesi itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye anakozuiliwa mjini Kampala. Kumekuwa na shinikizo kubwa kimataifa la kutaka Bobi Wine aachiwe huru.

Baada ya kuachiwa kwa Bobi Wine, Kiongozi wa Upinzani Kizza Besigye amekamatwa na polisi wakati akiondoka nyumbani kwake, eneo la Kasangati na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Naggalama, Kusini mwa Kampala.

The post Breaking News: Bobi Wine Aachiwa Huru, Besigye Akamatwa appeared first on Global Publishers.