NEWS

18 Agosti 2018

MAKONDA ASHIRIKI TAMASHA LA KOMAA CONCERT, AWAAHIDI MAKUBWA WASANII


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akihutubia maelfu ya wananchi waliofika kwenye tamasha hilo.

Wananchi waliofika kwenye tamasha hilo wakinyoosha mkono kuunga  kile alichokuwa amezungumza.

 

 

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo ameungana na maelfu ya wakazi wa jiji hilo kwenye Tamasha kubwa la Burudani lijulikanalo kama ‘Komaa Concert 2018’ lililoandaliwa na kituo cha utangazaji cha E FM/TV E ambapo amesema serikali ya mkoa wake itaendelea kutoa ushirikiano kwa wasanii kwakuwa sanaa ni ajira rasmi inayowasaidia vijana wengi.

 

 

Akizungumza na maelfu ya wananchi hao,  Makonda amewaomba waendelee kumpa ushirikiano wa kutosha Rais Dkt. John Magufuli huku akipongeza maendeleo makubwa yaliyopatikana tangu Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani.

 

Aidha amewapongeza E FM kwa kuandaa tamasha hilo lililotoa fursa kwa wananchi wanyonge kupata burudani huku akiwakumbusha wananchi kuhakikisha wanafanya usafi wa mazingira kwenye maeneo yao wanayoishi.

Pia amewahimiza wananchi kuhakikisha wanalinda Amani, usalama na kuwakumbuka kwenye maombi viongozi wote wa Taifa.

The post MAKONDA ASHIRIKI TAMASHA LA KOMAA CONCERT, AWAAHIDI MAKUBWA WASANII appeared first on Global Publishers.