WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknlolojia, Prof. Joyce Ndalichako amezindua mfumo wa masomo ya kielektroniki kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili kujifunza kwa njia ya Vikaragosi utakaowawezesha wanafunzi hao kujifunza kwa kutumia mifumo ya (Cartoon).
Prof. Ndalichako akizungumza katika hafla hiyo amepongeza Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na kueleza kuwa mfumo huo utawawezesha wanafunzi hao kuelewa masomo yao kwa ufanisi zaidi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Prof. Bernadeta Killian ameeleza kuwa uzinduzi huo ni wa awamu ya kwanza ukiwa na lengo la kuboresha ufundishaji na stadi za kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu.
Uzinduzi wa mfumumo huo wa kujifunza kwa kutumia vikaragosi utaongeza wigo na ari ya wanafunzi kupenda masomo yao huku ikiwa ni njia rahisi ya kuongeza maarifa kwa wanafunzi wa darsa la kwanza na la pili hapa nchini.
The post PROF. NDALICHAKO AZINDUA VIKARAGOSI KWA MASOMO YA DARASA LA 1 NA II appeared first on Global Publishers.