NEWS

20 Agosti 2018

MKWANJA WA DE BRUYNE SI MCHEZO

 

MAN­CHES­TER City im­epata tatizo kubwa kufuatia majeraha aliyopata supastaa wao fundi wa pasi za mwisho na mbunifu, Kevin De Bru­yne.

Mbelgiji huyo anaweza kuwa nje ya uwanja kwa miezi hadi mitatu baada ya kupata jeraha kubwa katika goti lake la kulia mazoezini na kusaba­bisha pigo kubwa kwa City msimu ukiwa ndiyo kwanza umeanza.

Lakini Kevin De Bruyne ni nani? Mpira umempa mafanikio gani kiuchumi? Hapa ni kila unacho­takiwa kujua kuhusu raia huyu wa Ubelgiji.

 

KEVIN DE BRUYNE NI NANI?

Kevin De Bruyne ni mwanasoka wa kulipwa anayeichezea Manchester City na timu ya taifa ya Ubelgiji.

Alizaliwa Ghent, Ubelgiji Juni 28, 1991. De Bruyne alianza soka lake la uto­toni na Klabu ya nyumbani kwao KVV Drongen kuanzia 1997 hadi 1999 kabla ya kuichezea Gent kuanzia 1999 hadi 2005, na Genk kuanzia 2005 hadi 2008.

 

Baadaye alianza soka la uku­bwani mwaka 2008 akiwa na Genk, na akaisaidia kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Ubelgiji msimu wa 2010-2011. Januari 2012, alijiunga Chelsea lakini alikuwa hatumiki mara kwa mara, hivyo akapelekwa kwa mkopo Werder Bremen kwenye Bundes­liga kuanzia 2012 hadi 2013.

 

De Bruyne baadaye alijiunga na Wolfsburg mwaka 2014 na kuwa na msimu wa mafanikio huko, ambako alitajwa kuwa Mwanasoka Bora wa Mwaka Ujerumani 2015 baada ya kufunga mabao 16 na kutoa pasi za mabao 27 ndani ya msimu mmoja.

 

Ubora aliouonyesha Ujerumani ulimwezesha kupata uhamisho wa rekodi Manchester City mwaka 2015, ambako aliisaidia timu hiyo kubeba ubingwa wa Pre­mier na Kombe la Ligi mara mbili. Haikuishia hapo, alitajwa kuwa Mwanasoka Bora wa Mwaka Man­chester City mara mbili 2016 na 2018.

Kwenye ngazi ya kimataifa, De Bruyne pia amepata ma­fanikio kadhaa. Tangu alipoanza kuichezea Ubelgiji 2010, amecheza jumla ya mechi 65 na kuiwezesha timu hiyo kwenye robo fainali ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil na Euro 2016 Ufaransa. Pia aliisaidia Ubelgiji kumaliza nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

 

DE BRUYNE ANA UMRI GANI?

Kevin De Bruyne na umri wa miaka 27. Alizaliwa Juni 28, 1991.

DE BRUYNE ANA UTAJIRI WA KIASI GANI?

Kwa mujibu wa Jarida la Celebrity Net Worth, utajiri wa Kevin De Bruyne in­aaminika kufikia pauni milioni 23.5 (Sh bilioni 68 na milioni 119).

 

 

DE BRUYNE ANATENGENEZAJE FEDHA?

Kama ilivyo kwa wachezaji wengi wa kulipwa, De Bruyne anapata fedha zake kutokana na mchanganyiko wa mikataba minono na dili za matangazo.

Alisaini mkataba mnono Chelsea Januari 2012 wa miaka mitano na nusu na baadaye akasaini Manchester City Agosti 2015 kwa dau la rekodi la pauni milioni 55 kwa miaka sita, na kumfanya kuwa mchezaji ghali namba mbili katika historia ya soka la England.

 

Kwa nyongeza, De Bruyne pia amepiga pesa nyingi sana za matangazo kwa miaka mingi maishani mwake, yakiwemo madili kutoka Nike na Orange.

MKE WA KEVIN DE BRU­YNE NI NANI?

Kevin de Bruyne amemuoa mrembo Michele Lacroix tangu Juni 2017. Wawili hao wana mtoto mmoja wa kiume aitwaye Mason Milian De Bruyne, aliyezaliwa Machi 10, 2016.

The post MKWANJA WA DE BRUYNE SI MCHEZO appeared first on Global Publishers.