
Luka Modric
KIUNGO wa Real Madrid, Luka Modric amefanikiwa kubeba Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya katika utoaji wa tuzo uliofanyika jana.
Modric aliwazidi Mohamed Salah wa Liverpool na C r i s t i a n o Ronaldo wa Juventus aliokuwa akiwania nao katika nafasi tatu za mwisho.
RAMOS USO KWA USO NA SALAH
Wakati utoaji wa tuzo ukiendelea, beki wa Real Madrid, Sergio Ramos alikuwa amekaa siti ya nyuma ya mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah ambaye walitibuana wakati wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.
Ramos alipita na kumgusa Salah begani wakati akitoka kuchukua tuzo, hali ambayo ilisababisha kamera nyingi kuwamulika wao, ikumbukwe kuwa Ramos alimchezea faulo Salah ambaye alilazimika kukaa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa na kushindwa kucheza hadi mwisho katika fainali ya Ulaya.
BECKHAM APATA TUZO
Staa wa zamani wa Manchester United, David B e c k h a m alipata tuzo maalum ya Rais wa UEFA kutokana na m c h a n g o wake kwenye mchezo wa soka, ambapo alikabidhiwa na kutoa hotuba fupi ya kushukuru.
TUZO NYINGINE
Mshambuliaji Bora: Cristiano Ronaldo
Kiungo Bora: Luka Modrić
Beki Bora: Sergio Ramos
Kipa Bora: Keylor Navas
The post Modric Mchezaji Bora Uefa appeared first on Global Publishers.