NEWS

18 Agosti 2018

Mwanasheria Mkuu wa CUF, Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam Wajiuzulu na Kuhamia CCM

Na Magdalena Kashindye
Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mussa Swedi Kafana Diwani wa Kiwalani na Mwanasheria Mkuu wa CUF - Maalim, Hashim Bakari Mziray wamejiuzulu uanachama CUF pamoja na nyadhifa zao zote na  kujiunga  CCM. 

Wamedai kuwa, wameamua kuhama kutokana na  Viongozi wa upinzani kuonyesha unafiki na kushindwa kushirikiana.

“Chama cha CUF kina pande mbili zinavutana, na mgogoro huu hauwezi kuisha leo wala kesho kwasababu wanaobishana na kuvutana ni watu wakubwa kwenye chama” amesema Kaffana na kuongeza;

"Migogoro ya chama cha CUF inaweza kuniharibia future yangu kisiasa na uongozi kwa ujumla hivyo kwa dhati ya moyo wangu pasipo kushawishiwa na mtu yoyote ninajivua uanachama na kuachia madaraka ya unaibu meya wa jiji la Dar es salaam pamoja na udiwani"