NEWS

20 Agosti 2018

NAY WA MITEGO AFUNGUKA ISHU YA KUFILISIWA NA BENKI

Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’

Staa wa Bongo Fleva, Emm-anuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameifungukia ishu ya kufilisiwa na benki inayosemekana inamdai baada ya kukopa na kushindwa kulipa. Nay aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, siyo kweli kwani mali zake zote zipo na hajawahi kuwa na mkopo kwenye benki yoyote.

Ishu ya Nay kufilisiwa ilianza kusambaa mitandaoni baada ya mashabiki kudai msanii huyo kwa sasa hana jipya kwani benki hiyo walik-wenda nyumbani kwake na kutaifisha mali zake zote zikiwemo nyumba na magari anayomiliki baada yakushindwa kulipa deni. Nay alisema hakuna ishu kama hiyo na hakuna mali yake yoyote iliyopigwa mnada kwa sababu mali zake zote zipo na hafikirii kwenda kukopa sehemu yoyote.

“Ni stori tu ambazo watu wameamua kuzungumza na watu kuzungumza siyo dhambi kwa sababu mimi ni staa, kwa hiyo watu wakiwa wanaongea vitu kama hivyo huwa sishtuki, nawaa-ngalia tu,” alisema Nay.

MEMORISE RICHARD

The post NAY WA MITEGO AFUNGUKA ISHU YA KUFILISIWA NA BENKI appeared first on Global Publishers.