NEWS

20 Agosti 2018

Picha: Shilole aonyesha Mjengo wa Jumba Lake

Msanii wa Bongo Fleva, Shilole ameonyesha nyumba yake anayojenga ambayo kwa sasa ipo katika hatua za mwisho kukamilika.

Muimbaji huyo ambaye amekuwa akijihusisha na mambo mbalimbali nje ya muziki ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwajuza mashabiki wake hilo.

"Mama Ntilie mie nikiwa katika harakati za kupambana kumalizia ili na mimi niitwe Mama mwenye Nyumba. Mjini pagumu haijawa rahisi lakini ashukuriwe Mungu Nilisema Ntakomaa na Jiji Mnyamwezi wa Igunga mimi," ameeleza Shilole.

Shilole alikuwa ni muuza soda na vitafunwa kwenye stand ya Mabasi, baadae akawa Msanii na sasa anaelekea kuwa miongoni mwa kina Mama wenye nyumba au wanaomiliki nyumba  Jijini Dar es salaam