Kuna picha aliweka Gadner akiwa amerepost kutoka katika akaunti ya binti yake Karen ikiwa inaonyesha akiwa amemkumbatia mtoto wake huku wakiwa wamelala kwenye kochi, na kwa jinsi wao walivyochukulia ilikuwa ni kama mapenzi ya baba na mtoto.
Lakini baada ya picha hiyo kwenda katika mitandao ya kijamii ilileta gumzo na kusemewa maneno mengi sana huku wadau na baadhi ya mashabiki wakisema kuwa hayo sio maadili ya kitanzania hasa kwa baba na binti yake.

