GEITA: Mwalimu wa shule ya Sekondari ya Bugando Kata ya Nzera wilayani Geita mjini hapa, Noel Seleman anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na denti wa kidato cha kwanza chumbani kwake.
Katika tukio hilo lililojiri hivi karibuni maeneo hayo, ticha huyo alidaiwa kuwa na uhusiano wenye shaka na mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 17, uhusiano unaoelezwa kudumu kwa takriban mwaka mmoja sasa.
Akisimulia tukio hilo, baba mzazi wa mwanafunzi huyo, Francis Andrea alieleza kusikitishwa kusikitishwa na kitendo cha mwalimu huyo huku akiiomba Serikali imsaidie.
“Ni muda nilikuwa nikisikia kuwa mwanangu ana uhusiano na mwalimu.
“Siku ya tukio aliondoka nyumbani asubuhi, niliporudi nyumbani nikamuuliza mama yake, akaniambia alimtuma, lakini jambo la kushangaza tangu saa nne asubuhi hadi saa nane mchana alikuwa hajarejea nyumbani ndiyo nikachukua uamuzi wa kumwambia mdogo wake ambaye alikuwa naye kuwa dada yake yupo wapi.
“Mdogo wake alinipeleka na kunionesha kuwa yupo chumbani kwa mwalimu wake, nilikasirika sana na kama mzazi nilicharuka.
“Nilirudi nyumbani kwa hasira, nikawachukua vijana sita na wanawake wanne tukaenda kumkamata huyo mwalimu baada ya kumkuta ‘laivu’ na binti yangu chumbani.
“Baada ya kumkamata tulimwita balozi wa eneo hilo akashuhudia na kutusaidia kumfikisha Polisi,” alisema baba huyo kwa uchungu.
Kwa upande wake, mama wa mwanafunzi huyo, Joyce Katambi aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, mara kwa mara amekuwa akimkanya binti yake kujihusisha na mapenzi akiwa bado anasoma, lakini amekuwa hamsikilizi, hali ambayo ilimsababisha kujikuta akikutwa na mwalimu wake chumbani.
Balozi wa eneo hilo, Shaaban Majaliwa alisema walipozungumza na mwanafunzi huyo alikiri kuwa na uhusiano na mwalimu wake.
Kwa upande wake mwanafunzi huyo alipohojiwa na Ijumaa Wikienda alikanusha kuwa na uhusiano na ticha wake na kwamba alikwenda nyumbani kwake kumjulia hali baada ya kupata taarifa kuwa amepata ajali.
Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, ACP Mponjoli Mwabulambo aliliambia gazeti hili kuwa, tukio hilo lilijiri Agosti 13, mwaka huu, majira ya saa nane mchana ambapo mtuhumiwa alitiwa mbaroni na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
STORI: MWANDISHI WETU, Wikienda
The post TICHA AKUTWA NA DENTI CHUMBANI appeared first on Global Publishers.