NEWS

22 Septemba 2018

Papa Fransisco Awalilia Waliokufa Kwenye Ajali MV Nyerere

Kiongozi wa Kiroho wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Papa Fransisco ametuma salamu za Rambirambi kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere.

Katika salamu zake kupitia kwa Balozi wake nchini Tanzaniia, Papa Francis ametoa pole wote walioko katika kipindi cha majonzi na kuwapa moyo wote wanaotafuta ndugu zao ambao mpaka sasa hawajaonekana.

 

Aidha, Papa Francis amemuomba Mungu awajalie baraka, nguvu na faraja wote walioguswa na msiba huo.

 

Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi mchana Septemba 20, 2018 imefikia 157  huku uokoaji ukiendelea.

MAGUFULI Awalilia Waliokufa Ajali ya Mv Nyerere/ Atoa Siku Nne

The post Papa Fransisco Awalilia Waliokufa Kwenye Ajali MV Nyerere appeared first on Global Publishers.