NEWS

22 Septemba 2018

Updates Kutoka Ukerewe: Miili Iliyookolewa Yafikia 157 – Video

TAARIFA tulizozipata kutpoka katika Kisiwa cha Ukara ambako ndipo miili ya Marehemu inapelekwa kwa ajili ya kutambuliwa na ndugu zao, idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi mchana Septemba 20, 2018 imefikia 157 na uokoaji bado unaendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema miili mingine imeopolewa leo asubuhi Septemba 22, 2018 na kwamba vikosi vya uokoaji vinaendelea na shughuli ya uokoaji na ikitarajiwa shughuli hiyo kufanyika hadi kesho Jumapili.

“Hadi jana (Ijumaa Septemba 21, 2018) miili 116 imeshapata ndugu na tunaamini miili mingine itatambulika maana wananchi wanaendelea kuwasili kuja kuitambua,” amesema Mongella.

MAGUFULI Awalilia Waliokufa Ajali ya Mv Nyerere/ Atoa Siku Nne

The post Updates Kutoka Ukerewe: Miili Iliyookolewa Yafikia 157 – Video appeared first on Global Publishers.