HII ikufikie wewe mpenda kunata na midundo huku unaangalia mashairi kwenye TV kuuubwaaaa! Ipo hivi; Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar unatarajiwa kufanya usaili mkubwa leo wa kumtafuta mkali wa kuimba Karaoke 2018 ambapo mshindi atatunzwa zawadi kubwa ikiwemo ofa ya kurekodi na kusimamiwa muziki wake.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’ alisema kuwa, usaili huo utaanza mapema leo kuanzia saa 12 za jioni na kuendelea.
“Niwaombe tu, vijana wote wa wilaya zote kufika kwa wingi Dar Live kwa ajili ya kufanyiwa usaili, tunatarajia kuanza usaili mapema kuanzia saa 12 za jioni na kuendelea, hivyo njoo ufanye usaili na tukijua kuwa unaweza basi utakuwa umeingia moja kwa moja kwenye shindano letu,” alisema KP na kuongeza kuwa usaili huo utakuwa buree kabisa.
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na wahusika kupitia namba; 0759 915 692/ 0716 204 245.
The post Usaili Mkubwa Wa Karaoke Kufanyika Leo Dar Live appeared first on Global Publishers.