NEWS

16 Septemba 2018

Victoire Ingabire na Kizito Mihigo Waachiliwa Huru Rwanda

Victoire Ingabire.

Mwanasiasa wa upinzani nchini, Rwanda, Victoire Ingabire,  ameachiwa huru leo Jumamosi kufuatia baraza la mawaziri nchini humo kuidhinisha amri ya ‘huruma’ ya Rais lilipokutana jana Ijumaa. Ingabire ameachiwa sambamba na wafungwa wengine 2,140.

Mbali na Ingabire ni mwanamuziki Kizito Mihigo ambaye alifungwa kwa miaka 10, 2015 kwa kupanga njama za kumuua rais Paul Kagame.

Mwanamuziki Kizito Mihigo

Alipokuwa akitoka jela, Ingabire alimshukuru rais Kagame, akisema huu ndio mwanzo wa kufunguka kwa sehemu ya kisiasa nchini Rwanda, kulingana na shirika la AFP.

Lakini waziri wa haki Johnston Businge alipuuzilia mbali umuhimu wa kuachiliwa kwa bi Ingabire.

”Hakuna chochote cha kisiasa kuhusu kuachiliwa kwake-na hakuna chochote cha kisiasa kuhusu kufungwa kwake”, aliambia Reuters.

 

 

 

BBC news

The post Victoire Ingabire na Kizito Mihigo Waachiliwa Huru Rwanda appeared first on Global Publishers.