NEWS

16 Septemba 2018

Wasomaji Wafurahia Bei Mpya ya Sh. 500 ya Spoti Xtra

GAZETI la Spoti Xtra limekuja katika ujio mpya unaohusisha  punguzo la bei  ambapo kuanzia leo (Jumapili) linauzwa kwa Sh. 500 tu badala ya Sh. 800 iliyokuwepo awali na litakuwa linatoka mara mbili kwa wiki — Alhamisi na Jumapili.

Uzinduzi wa punguzo la bei umefanyika leo ambapo timu ya gazeti hilo la Spoti Xtra ilitembelea wasomaji wake  maeneo ya  Tabata-Kinyerezi, Segerea,  Vingunguti, Ubungo, Mwenge na sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam ambapo magazeti yalitolewa bure.

Baada ya timu ya promosheni ya Spoti Xtra kutembelea wasomaji sehemu hizo, wasomaji hao walitoa pongezi kibao kwa maombi waliyoyatoa kuhusu kupunguziwa bei kwa gazeti hilo.

 

Ili kujishindia zawadi hizo, msomaji anatakiwa kununua gazeti la Spoti Xtra siku ya Alhamisi na Jumapili  ambapo utatakiwa kujaza kupoeni iliyomo ndani ya gazeti hilo kwa kufuata maelekezo yaliyomo.

Uongozi wa Spoti Xtra umedhamiria kufanya mabadiliko makubwa ya kuliboresha gazeti na wasomaji wake wakae mkao wa kupata burudani ya kutosha.

Wasomaji wa gazeti la Spoti Xtra wa Tabata-Segerea, wakifuatilia habari za michezo na burudani katika gazeti hilo.

Wasomaji wa Spoti Xtra wakiburudika na stori zake.

Msomaji (kulia) akipata maelekezo kutoka kwa Ofisa Masoko wa gazeti la Spoti Xtra, Jimmy Haroub.

Wasomaji wakifurahia uhondo wa Spoti Xtraleo huko Vingunguti, jijini Dar es Salaam.

Msomaji akipata chakula na kusoma Spoti Xtra.

Muuza mihogo maeneo ya Ubungu akijinafasi na Spoti Xtra.

Muuza matunda wa Mwenge akufuatilia kwa makini uhondo wa Spoti Xtra.

 

The post Wasomaji Wafurahia Bei Mpya ya Sh. 500 ya Spoti Xtra appeared first on Global Publishers.