MWANAMUZIKI wa kike ambaye aliweka kionjo cha sauti katika Wimbo wa Nitarejea wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Hawa Mayoka ‘Hawa Nitarejea’, hatimaye amepelekwa nchini India kwa matibabu ya tatizo la ini lililokuwa likimsumbua kwa muda mrefu.

Gharama zote za matibabu ni chini ya Diamond ambaye mbali na kushirikiana naye kimuziki, pia aliwahi kudaiwa kuwa mpenzi wake.
Akizungumza kwa furaha wakati akiondoka nchini wikiendi iliyopita, Hawa alisema kuwa anaamini kabisa ndoto yake ya kupona inaenda kutimia maana ameteseka kwa muda refu bila kujua msaada wake wa kupata matatibu utatoka wapi kwa sababu alishakata tamaa ya kupona.

Hawa alikuwa amefikia katika hali mbaya hivyo kujitolea kwa Diamond kumlipia matibabu kumeokoa maisha yake.
“Unajua mtu siku zote ukisema sana unaweza kukufuru kabisa, lakini kwa kitu alichofanya Diamond ni Mungu pekee ndiye wa kuweza kumlipa kwani ameokoa maisha yangu ambayo nilikuwa nimeshakata tamaa kabisa hata ya kuendelea kuishi, lakini Mungu ni mwema ninaenda kupata matibabu sasa,” alisema Hawa muda mchache kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti matumizi ya madawa ya kulevya cha Pillmissan Foundation kilichopo Kigamboni, Pilli Missana alisema kuwa anamshukuru Diamond kwani ameonesha moyo wa kipekee na wa utu kwa kumsaidia Hawa na anamuomba Mungu ampe nguvu zaidi na uwezo wa kuwasaidia wengine ambao hawana.
Kwa muda mrefu Hawa amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa ini uliomsabishia tumbo kujaa maji.
EXCLUSIVE Alikiba: “Kutekwa kwa MO Dewji Nimeguswa Sana”
The post Hatimaye Diamond Ampeleka India, Hawa Nitarejea appeared first on Global Publishers.