NEWS

14 Oktoba 2018

Rais Magufuli na Mkewe Wamtembelea Maria Nyerere

RAIS John Magufuli na mkewe Janeth Magufuli leo wamemtembelea mke wa hayati Mwalimu Julius Nyerere, Maria Nyerere,  nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam baada ya kuhudhuria misa maalumu kumuombea Baba wa Taifa, Julius  Nyerere,  iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oyster Bay jijini Dar es Salaam leo Jumapili Oktoba 14, 2018.

Rais  John Magufuli na mkewe,  Janeth Magufuli,  wakiwa na waumini wengine katika Ibada Maalumu ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba 14, 2018

Rais  Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakitoa sadaka walipoungana na waumini wengine katika Ibada.

Rais Magufuli akinunua Rosari baada ya kuhudhuria Ibada Maalumu ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Rais  Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakiwa na Mama Maria Nyerere na mwanae Makongoro Nyerere walipomtembelea nyumbani kwao Msasani jijini Dar es salaam baada ya kungana na waumini katika Misa Maalumu kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba 14, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mjane wa Baba Taifa, Mama Maria Nyerere, aliyemtembelea nyumbani kwake Msasani baada ya kutoka katika Ibada Maalumu ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba 14, 2018

Mama Janeth Magufuli akimsalimia Mama Maria Nyerere.

The post Rais Magufuli na Mkewe Wamtembelea Maria Nyerere appeared first on Global Publishers.