Mkurugenzi wa ILUS, Lugendagenda Philipo akisaini kitabu cha wageni. Anayemfuata ni Sosthenes Robert, Mabula Ilaga na Lyadunda Mkang’u. Aliopo nyuma ni Samson Gaganija.
Stori: Mwandishi Wetu
WAHITIMU wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambao wameanisha kampuni yao ubunifu na usanifu iitwayo ILUS, jana wametembelea Kampuni ya Global Publisher iliyopo maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar na kujionea shughuli mbalimbali za uandaaji wa magazeti na Global TV.
Whitimu hao wakipanda ngazi kuelekea magazeti Pendwa.
Wakiwa Global, wahitimu hao ambao walianzisha kampuni hiyo kabla hawajahitimu masomo kwa kutumia fedha za kujikimu (boom), waliweza kutembelea vitengo mbalimbali vya kampuni hiyo.
Walianzia kwenye magazeti Pendwa; Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Risasi Jumamosi ambapo waliweza kubadilishana mawazo na baadhi ya wahariri kisha wakapita katika kitengo cha usambazaji.
Mhariri wa Championi Jumamosi, Lucy Mgina (katikati) akisalimiana na Lugendagenda huku wafanyakazi wa ILUS na Mhariri wa Amani, Erick Evarist wakifurahia jambo.
Pia waliweza kufika kwenye kitengo cha magazeti ya michezo ya Championi pamoja na Spoti Xtra na Global TV.
“Tunashukuru sana kwa ziara hii, lengo la sisi kuja hapa ni kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa Mkurugenzi Eric Shigongo ambaye historia yake tunaifahamu ni ya kuanzia chini kama sisi ambavyo tumeanzisha ILUS tukiwa angali bado tupo chuoni,” alisema Ofisa Mahusiano wa Kampuni ya ILUS, Lyadunda Mkang’u.
Lugendagenda akisalimiana na mwandishi mwandamizi, Imelda Mtema (aliyekaa). Kulia ni Mabula na Sosthenes. Kushoto ni Mhariri wa Gazeti la Amani, Erick Evarist.
Naye Mhariri Mtendaji wa Global, Saleh Ally, aliwapongeza vijana hao kwa kuungana na kuanzisha kampuni yao ambayo tayari imeajiri vijana wengine 11 na kuwataka kuwa makini kwani mara nyingi mafanikio yanapokuja, wanaweza kujikuta wanaanza kutofautiana.
Wafanyakazi wa ILUS wakiwa katika picha ya pamoja na Mhariri Mtendaji wa Global, Saleh Ally (wa nne kutoka kushoto).
“Hongereni kwa kuanzisha kampuni, niwatie moyo tu kwamba mnaweza kufika mbali zaidi lakini tu muwe makini maana kampuni nyingi zinazoanzishwa na vijana hivi huwa matatizo yanatokea pale mtakapoanza kupata mafanikio,” alisema Saleh.
Kupitia kampuni yao, wasomi hao wameweza kufanya kazi mbalimbali za ubunifu wa vitabu, logo na mabango makubwa. Wamefanya pia kazi nyingi na Serikali.
PICHA: RICHARD BUKOS/GPL
The post WAHITIMU WA CHUO CHA NIT WATEMBELEA GLOBAL appeared first on Global Publishers.