NEWS

11 Novemba 2018

MREMBO SUDAN AOLEWA KWA NG’OMBE 520, TOYOTA 3 KALI

Nyalong na mumewe Kok Alat siku ya ndoa.

HATIMAYE familia ya mrembo wa Sudan ya Kusini aliyekuwa anagombewa na waposaji kibao walioahidi kutoa mahali kubwa zisizo za kawaida, ameolewa kwa mahari ya ng’ombe 520 na magari matatu aina ya Toyota V8!

Mrembo Nyalong Ngong Deng (17) kutoka eneo la Awerial, alikuwa na wachumba sita waliokuwa wanamtaka na kila mtu alikuwa tayari kutoa mahali bab’kubwa ikiwa ni pamoja na Sh. milioni moja za Kenya ambazo ni sawa na Sh. milioni zipatazo 20 za Tanzania!

Akiwa amekaa kwa utulivu kando ya mumewe, tajiri mkubwa aitwaye Kok Alat katika ukumbi wa Freedom Hall jijini Juba, Ijumaa iliyopita, Novemba 9, Nyalong, mrembo wa kabila la Dinka,  alikuwa nadhari ya mshangao uliowapata watu waliokuwa katika sherehe hiyo.

 

Image result for Nyalong Ngong Deng

Nyalong akiwa nyumbani kwao; na baba na nduguze kabla ya ndoa.

Image result for Nyalong Ngong Deng

Nyalong, mumewe.

 

The post MREMBO SUDAN AOLEWA KWA NG’OMBE 520, TOYOTA 3 KALI appeared first on Global Publishers.