NEWS

31 Desemba 2018

Hisia kali zatolewa baada ya rais wa Ufilipino kuelezea alivyomnyanysa kingono yaya

Hisia kali zatolewa baada ya rais wa Ufilipino kuelezea alivyomnyanysa kingono yaya
Kumekuwa na msururu wa ukosoaji baada ya rais wa Philipino Rodrigo Durtete kusema kuwa alimnyanyasa kingono yaya mmoja wakati alipokuwa kijana.

Katika hotuba yake , alikiri kutoa ushuhuda mbele ya padri vile alivyoingiza mkono wake ndani ya suruali ya yaya huyo alipokuwa amelala.

Mwanaharakati wa makundi ya haki za kibinaadamu Gabriela alisema bwana Durtete hakustahili kuwa katika wadhfa huo na kwamba angefaa kujiuzulu.


Rais huyo wa Ufilipino amezua hisia kali kutokana na matamshi yake machafu lakini ameendelea kuwa maarufu. Katika matamshi yake ya hivi karibuni , alielezea kuingia katika chumba cha yaya huyo aliyekuwa amelala.

''Nilinyanyua blanketi .... na kujaribu kushika kile kilichokuwa ndani ya suruali yake ya ndani'' , alisema.

''Nilikuwa namgusa . Aliamka na hivyobasi nikatoka katika chumba hicho''.

Anasema kwamba baadaye alimwambia kuhani kwamba baadaye alirudi katika chumba cha mwanamke huyo na kujaribu kumnyanyasa tena.

Durtete amesema kwamba padri huyo alimwambia kusoma ibada tano za ''baba yetu aliye mbinguni na Maria mtakatifu kwa sababu ataenda motoni iwapo singefanya hivyo, kulingana na tovuti moja kwa jina Rappler.

Ni jambo la kawaida kwa familia tajiri nchini Ufilipino kuwaajiri yaya na wanawake wengi hufanya kazi kama wasaidizi wa nyumbani katika eneo la bara Asia na mashariki ya kati.

Msemaji wa Durtete hadi kufikia sasa anasema kuwa alitunga habari hiyo na kutia chumvi wakati wa hotuba yake siku ya Jumamosi.

Makundi ya wanaharakati nchini Ufilipino yameshutumu matamshi hayo ambayo yalitolewa, ikiwa ni miongoni mwa mashtaka dhidi ya kanisa katoliki kuhusu unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto

Gabriela, mwakilishi wa wanawake katika makundi ya haki za kibinaadamu alisema kuwa matamshi hayo ni sawa na kukiri kutekeleza ubakaji.


Duterte aidhinisha sheria ya kijeshi Mindanao
Muungano dhidi ya ulanguzi wa wanawake hadi eneo la Pacific mwa bara la Asia ulionya kuwa matamshi ya rais huyo yanawaweka wafanyikazi wa nyumbani katika hatari.

''Ubakaji haufanyiki kupitia kuingiza uume katika uke pekee'', katibu mkuu was shirika hilo Joms Salvador alisema. ''Iwapo ni kidole ama kitu chochote hutajwa kuwa ubakaji''.

''Kufanya vitu vya kunyanyasa kunashawishi vitendo vya ubakaji na katika kisa hiki, unyanyasaji wa kingono dhidi ya wafanyikazi wa nyumbani'', alisema mkurugenzi mkuu Jean Enriquez.

Zaidi ya raia milioni moja wa Kifilipino hufanyakazi ughaibuni kama mayaya kulingana na takwimu za serikali. Bwana Durtete amekuwa mkosoaji mkuu wa kanisa katoliki ambalo limekosoa vita vyake dhidi ya dawa za kulevya ambavyo vimesababisha mauaji ya maelfu ya raia.