NEWS

31 Desemba 2018

JPM APONGEZWA , ATAKIWA KUWA IMARA

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uongozi wa Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mwaka 2014, Mnawaru Hamudi ambaye pia ni mwanaharakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).

 

 

ALIYEKUWA Waziri Mkuu wa Uongozi wa Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mwaka 2014, Mnawaru Hamudi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kutokana na utendaji wake uliotukuka.

Akizungumza na waandishi wa habari Hamudi ambaye pia ni mwanaharakati amesema kuwa rais Magufuli anapaswa kuungwa mkono kutokana na utendaji wa kuhakikisha raslimali za nchi zinalindwa na watanzania wananufaika nazo.

 

Amesema kuwa Magufuli amekuwa kiongozi wa kipekee katika kuhakikisha anatimiza ahadi zake kwa wakati na kupambana na mafisadi ambao walikuwa kazi yao ni kula jasho la watanzania wazalendo.

 

Aidha Hamudi amewaomba watanzania kumwombea mama mzazi wa Rais Magufuli  Suzana Magufuli ambaye anapatiwa matibabu hapa jijini Dar es Salaam aweze kupona na kurejea katika hali yake ya zamani.

The post JPM APONGEZWA , ATAKIWA KUWA IMARA appeared first on Global Publishers.