IMEFICHUKA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mama wa mwanamuziki Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ kufunguka siri ambayo hajawahi kuisema popote, kwamba katika ukuaji wa mwanaye alikuwa anapenda sana kula kuliko shule.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda , mama wa mrembo huyo alisema kipindi Lulu anasoma shule ya msingi alikuwa anapenda kumfungia chakula ili aende nacho shule lakini matokeo yake alikuwa akifika shule anaanza kula kile chakula, kikiisha kabla ya masomo anarudi nyumbani bila kuingia darasani.
“Huyu Lulu alinisumbua sana, huwezi kuamini alikuwa anapenda kula kuliko masomo, nilikuwa nikimuandalia ‘paseli’ ya chakula kwa ajili ya kula ikifika mapumziko shuleni lakini cha kushangaza yeye alikuwa akila kabla na kikiisha anarudi nyumbani.
Stori: Na Memorise Richard
The post Mama: Lulu Diva Alipenda Sana Kula Kuliko Kusoma appeared first on Global Publishers.