NEWS

31 Desemba 2018

Simba Yaamua Kupeleka Kikosi Kamili Mapinduzi Cup

Simba yaamua kupeleka kikosi kamili Mapinduzi Cup
Klabu ya soka ya Simba inatarajia kusafiri Jumatano ya wiki hii ya tarehe 2/01/2019 kuelekea Visiwani Zanzibar kwaajili ya michuano ya kombe la Mapinduzi itakayoanza hivi karibu.


Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari Simba imesema kuwa itapeleka kikosi kamili kwenye mashindano hayo yanayofanyika kwaajili ya sikukuu ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.