Hapa bongo kumekua na tabia mtu akifanya kitu cha kichizi chizi ama kupatwa na uchuzi anadhaniwa kavuta bangi, Je wanaodhania hivyo wanakuwaga na ushahidi mtu kafanya kitu cha kichizi ama kawa chizi kwasababu ya bangi?.
Mtu anaweza kuwa chizi kwa msongo wa mawazo, malaria kupanda, kulogwa, n.k?
Binafsi nimesomea chuo Arusha na nimeshuhudia kuona watu wanaojielewa, wenye hekima na wenye mafanikio makubwa wakivuta bangi katika nyakati na maeneo tofauti tofauti.
Binafsi nilivuta bangi baada ya kushauriwa niache kuvuta sigara ambayo inaweza kukupa kansa ya mapafu au koo na hatimae kufa, Kwa sasa nimeacha kwasababu nipo mkoa flani ambao bangi ni adimu sana.
Ingekua bangi inaleta uchizi hivi kina snoop dogg na wiz khalifa wangebaki salama????