Kikosi cha Yanga kimeondoka leo kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki michuano ya kombe la mapinduzi iliyoanza kutimua vumbi januari mosi.
Akizungumza na Global TV Kocha Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila amesema kuwa ni mechi muhimu kwao na Imani kubwa ambayo wanayo ni kupata matokeo mazuri.
Aidha Mwandila amesema wachezaji ambao wameenda kuiwakilisha Yanga wana Imani nao na watafanya vizuri kutokana na baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza kukosekana huku wengi wao na matatizo mbalimbali.
Yanga ambayo ipo Kundi B inatarajia kushuka dimbani januari 3 dhidi ya KVZ huku timu nyingine zilizo kundi moja ni pamoja na Azam, Malindi na Jamhuri ya Pemba na kwa upande wa Simba inayotarajia kushuka dimbani janauri 4 dhidi ya Chipukizi ipo kundi A ikiwa pamoja na timu nyingine za KMKM na Mlandege.
The post YANGA Walivyoondoka na Kikosi B Kuelekea Zanzibar – VIDEO appeared first on Global Publishers.