NEWS

31 Machi 2019

DC KISARAWE ANENA BAADA YA HARAMBEE YA “TOKOMEZA ZERO”

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.

 

BAADA ya kufanyika kwa kampeni kabambe ya Tokomeza Ziro iliyolenga kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana wilayani Kisarawe, mkoani Pwani iliyofanyika  Machi 30, 2019  katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, chini ya mkuu wa wilaya hiyo, Jokate Mwegelo, mkuu huyo ametumia mtandao wa kijamii wa Instagram kufikisha ujumbe ufuatao:

NIMERUDI!!

Hakuna maneno Muhimu na Machache katika ustawi wa maisha ya Binadamu kama Tafadhali, Asante na Samahani.

Katika Dhifa niliyoiandaa jana, nilialika watu wengi, Wanasiasa, Taasisi za Kiserikali, Mabalozi, Wafanyabiashara, Wajasiriamali, Wasanii, Wadau wa Burudani N.k.

Na Makusudio ya yote hayo wote tunayajua, ni kutafuta MOTISHA juu ya ELIMU ya Mtoto wa kike, Kisarawe na kote nchini.


Na kwangu mimi na Wilaya nzima ya Kisarawe wote waliofika jana ni muhimu sana sana kwangu na kwetu.
Kipekee kabisa nimshukuru @officialpiere_liquid wako watu maarufu wengi mno tuliowaalika lakini hawakufika. Ila wewe ulichukua muda wako kuhamasisha na kufika na zaidi ya hapo ukatoa mchango wa TSH LAKI MOJA!!!

Hukuja kuuza sura tu!! Nasema ASANTE SANA. Wana Kisarawe tunakupenda na tunakukaribisha kuwekeza Kisarawe uanzishe hata mgahawa tutakusaidia kupata eneo.

Lakini pia nimesikia ni mtengenezaji mzuri sana wa furniture. Hii Shule tunayoenda kujenga inahitaji madawati Naomba tufanye kazi na wewe katika hii fursa. Tuangalie namna japo kidogo tukuwezeshe.


Tunasema Karibu Kisarawe Ukae. Kisarawe Kunogile. Tunasema Samahani kwa kukwazika lakini zaidi Asante Sana kwa kushiriki kwenye #TokomezaZeroKisarawe #ElimuItabakiKuwaJuuKileleni #KisaraweMpya
Ubarikiwe!!!!’

The post DC KISARAWE ANENA BAADA YA HARAMBEE YA “TOKOMEZA ZERO” appeared first on Global Publishers.