NEWS

2 Aprili 2019

Breaking News: Bunge Lakataa Kufanya Kazi na CAG

Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  Profesa Musa Assad.

BUNGE leo, Aprili 2, 2019, limepitisha hoja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki,  Kinga na Maadili ambayo ilitoa mapendekezo ya kutofanya kazi na Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Assad.

Taarifa iliyosomwa mapema leo bungeni na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka,  ililiomba bunge lipitishe azimio la kutofanya kazi na Mthibiti mkuu wa serikali ambapo azimio hilo lilipitishwa.

Wakati wa kusoma taarifa hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo amesema kuwa Profesa Musa Assad alikiri kuwa alisema bunge ni dhaifu na kwamba bado ataendelea kutumia maneno hayo kwa kuwa ni maneno ya kihasibu anayoyatumia kila siku na aligoma kuomba msamaha.

Mjadala unaendelea.

The post Breaking News: Bunge Lakataa Kufanya Kazi na CAG appeared first on Global Publishers.