NEWS

2 Aprili 2019

Watu 28 Wakamatwa kwa Kupiga Askari

WATU 28 wamekamatwa na polisi wilayani Nyang’hwale, Geita kwa tuhuma za kuwajeruhi askari polisi watatu kwa silaha za jadi wakati askari hao wakizuia wananchi wenye hasira kumshambuliwa mtu aliyedhaniwa ni mwizi.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatatu Aprili mosi 2019 kamanda wa polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amethibitisha askari wake kujeruhiwa na kuwataja waliojeruhiwa kuwa ni Omari ambaye ni mkaguzi wa Polisi tarafa ya Nyangwale.

 

Mwingine ni askari H16 D/C Yusuph aliyejeruhiwa mguu wa kulia na H4311 D/C Joseph aliyelazwa chumba cha uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.

 

Akielezea tukio hilo, Mponjoli amesema Jumamosi Machi 30, 2019 kundi la majambazi wakiwa na silaha za jadi walivamia nyumba za wakazi wawili kijiji cha Nyijundu na kumuua mkazi mmoja na kujeruhi wengine watatu kisha kupora fedha.

 

Amesema kufuatia hali hiyo, wananchi walipiga yowe na kuanza msako kwa kushirikiana na polisi na walipomkamata mmoja waliyedhani ni mtuhumiwa na kumhoji kisha kukiri walitaka kumuua na walipozuiwa na polisi wakawageuzia kibao.

The post Watu 28 Wakamatwa kwa Kupiga Askari appeared first on Global Publishers.