NEWS

2 Aprili 2019

Godbless Lema Atakiwa Kuripoti Kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge.....Wabunge wa CHADEMA Wasusa na Kutoka Nje ya Bunge

Naibu Spika wa Bunge, Dr Tlia Ackson amemtaka Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuripoti kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutokana na kauli yake kuwa "Bunge ni dhaifu". 

Lema ametoa kauli hiyo leo Aprili 2, 2019  Bungeni baada ya Ya Kamati ya Maadili ya Bunge Kumtia Hatiani Mdhitibi na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali,Profesa Mussa Assad na kutaka Bunge Lisishirikiane naye.

"....na mimi Nathibitisha Bunge hili ni Dhaifu "Amesema Lema

Kutokana na Maamuzi hayo ya Naibu Spika, Wabunge wote wa CHADEMA na Baadhi ya Wabunge wa CUF wametoka nje ya ukumbi wa Bunge